JWTZ Washusha Abiria Kwenye Magari yao na Bodaboda ili Washiriki Zoezi la Usafi


KATIKA hali isiyo ya kawaida, askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) Mkoani Mtwara jana walisimamisha vyombo vya usafiri barabarani asubuhi na kushusha abiria waliokuwemo, ili washiriki kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi.

Mwandishi alishuhudia abiria wakishushwa katika magari, pikipiki katika maeneo mbalimbali ya mji wa Mtwara na kutakiwa kushiriki zoezi la usafi.

Ufanyaji usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi umekosa mwamko mjini Mtwara tangu kuzinduliwa na Rais Desemba 9, mwaka jana.

Bila kujali itikadi za vyama wala cheo cha mtu, JWTZ waliwataka wananchi kupaki vyombo vya usafiri na kufanya usafi ili kukabiliana na milipuko ya magonjwa.

Baadhi ya wananchi walioshiriki usafi huo, walipongeza jitihada za JWTZ katika kutilia mkazo zoezi la usafi mkoani humo.

Zoezi hilo la usafi liliongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Halima Dendego ambaye alisema litakuwa endelevu mkoni hapo.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment