Isabela Afunguka 'Inaniuma Sana Kalama Kuniacha Mimi na Kumuoa Shoga Yangu'


SIKU chache baada ya Mbongo Fleva, Kalama Bakari ‘Luteni Kalama’ kuvuta jiko, hatimaye, aliyekuwa mchumba wa muda mrefu wa msanii huyo ameibuka na kusema anaumia kuona aliyeolewa alikuwa ni rafiki yake wa karibu.

Kalama alimuoa binti aitwaye Aisha Yassin wiki iliyopita ambapo saa chache baada ya ndoa hiyo kufungwa na picha kusambaa mitandaoni, wapenda ubuyu waliibuka na kuanza kueleza kuwa Kalama ameona shosti wa Isabela.

“Hili jambo sio siri limetuacha midomo wazi sisi tunaowajua vizuri hawa watu, walikuwa wanajifanya shemeji shemeji huku wanazima taa, isitoshe kwanza nasikia ana mtoto wa mwaka mmoja, yani ni majanga tupu, bora angemuachia Isabela aendelee na mtu wake waliyetoka mbali,” alisema mdaku mmoja.

Akiizungumzia ishu hiyo, Isabela alisema ameumia kuona Kalama amekwenda kwa rafiki yake kwani bora angemchukua mtu mwingine.

Luteni Kalama akiwa na Mkewe wa zamani, Isabela Mpanda

“Nimeumia. Rafiki yangu wa damu ambaye alikuwa anakuja tunakunywa wote na akionyesha kumheshimu Kalama kama shemeji yake eti leo kanigeuka, hii yote sababu yule mwanaume naye anapenda kulelewa halafu yule demu kidogo yupo vizuri kifedha.

“Japo nilikuwa nimeshamuacha Kalama kwa kuwa niliona ananipotezea muda, niliumia sana kwamba kwa nini awe rafiki yangu? Mungu atawaadhibu,” alisema Isabela.

Alipotafutwa Kalama na kusomewa mashtaka ya Isabela, alisema mwandani wake huyo wa zamani kakosa cha kuongea yeye aliachana naye kwa kuwa walishindwana na wala huyo mke wake hakuwa rafiki yake.

“Anatapatapa tu Isabela, ninachofahamu mimi ndio mume halali wa Aisha, kuhusu kuwa rafiki yake wala Bela hamjui huyo mwanamke vizuri, sioni cha ajabu kuoa mtu mwenye mtoto, atuache tufurahie maisha ya ndoa,” alisema Kalama.
SHARE

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment